WINGA wa Manchester United, Angel di Maria ameshinda Tuzo ya Mchezaji Bora Anayecheza nchini Argentina, kutoka Waandishi wa Habari nchini humo.
Di Maria, ambaye alijiunga na kikosi cha Louis van Gaal kwa dau la rekodi klabu, Pauni Milioni 60 msimu huu, ameshinda Olimpia de Plata katika sherehe zilizofanyika juzi baada ya kumpiku, Lionel Messi wa Barcelona.
Di Maria aliiwezesha klabu yake ya zamani, Real Madrid kutwaa taji lake la 10 Ulaya Mei mwaka huu na Argentina kufika Fainali ya Kombe la Dunia ambayo hakucheza kwa kuwa majeruhi na timu ikafungwa na Ujerumani.
Mchezaji huyo mtanashati amekuwa na
mwanzo mzuri katika soka ya England.
Angel Di Maria ameshinda tuzo ya waandishi wa Habari Argentina
Hii ni mara ya kwanza Lionel Messi anakosa tuzo hiyo tangu mwaka 2006

Chapisha Maoni