0

Mshambuliaji mpya wa Simba, John Bocco yuko Afrika Kusini kuikiongezea nguvu kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania’Taifa Stars’ ambacho kinashuka dimbani kesho Jumatano kumenyana na Zambia kwenye nusu fainali ya mashindano ya Cosafa.
Bocco ameitwa na kocha Salum Mayanga kuchukua nafasi ya Mbaraka Yusuph na Shana Chilunda ambao ni majeruhi.
Mayanga alisema licha ya kumjumuisha Bocco kwa ajili ya mashindano hayo lakini kubw ani kwa ajili ya mchezo wa kufuzu kwa fainali za Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ndani(Chan) dhidi ya Rwanda utakaofanyika Julai 15.
Mchezo huo umepangwa kufanyika kwenye Uwanja wa CCM Kirumba Mwanza na mshindi wa jumla wa mechi hiyo atapambana na Uganda


Chapisha Maoni

 
Top