0
Mahakama ya uhalifu ya kimataifa (ICC)
yenye wanachama 122 imeanza mkutano wake huku zingatio likiwa ni bara la Afrika, na huku ikiandamwa na kivuli cha kufutwa kwa kesi dhidi ya Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta.

Mkutano huo ulioanza jana unafanyika
siku tatu tu baada ya mwendesha
mashtaka mkuu wa mahakama hiyo yenye makao yake makuu mjini The Hague Fatou Bensouda, kufuta mashtaka dhidi ya Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta. 

Bensouda aliishutumu Kenya kwa kile alichosema ni kuzuwia uchunguzi wake, huku akikosolewa vikali na baadhi ya waafrika ambao wanasema ICC inaliandama bara hilo pekee, tangu ilipoundwa mwaka 2002.

Sura mbaya ya Afrika kuhusu mahakama ya ICC
Rais mpya wa Baraza la mataifa
wanachama wa mahakama hiyo Sidiki
Kaba alitowa wito wa maridhiano ya
kanda zote na hasa bara la Afrika. Katika
hotuba yake ya ufunguzi alisema
wanachama wa ICC wanapaswa kubadili
sura mbaya ya Afrika kuhusu mahakama
hiyo. Akasisitiza kwamba malalamiko
yanapaswa kusikilizwa, ingawa kuna yasio halali wala msingi madhubuti. 

Kaba ambaye ni Waziri wa sheria wa Senegal, alisema Afrika haiwezi kubakia zingatio pekee la mahakama hiyo.

Akakumbusha kwamba mwendesha
mashtaka mkuu na mahakimu wanne ni
kutoka bara la Afrika, na kuwa Congo,
Uganda,Jamhuri ya Afrika kati, Cote
dÍvoire na Mali zote ziliiomba mahakama ichunguze maovu yaliotendeka katika nchi hizo.

Balozi wa Kenya Macharia Kamau alilitaka baraza hilo kuyashughulikia malalamiko ya nchi yake na Umoja wa Afrika. 

Kenya imeataka kuwepo na mashauriano kuhusu mwenendo wa mahakama na Bibi Bensouda katika kesi dhidi ya Rais Kenyatta na Makamu wake Wiliiam Ruto juu ya madai ya kuhusika katika machafuko ya baada ya uchaguzi wa Disemba mwaka 2007.

Katika kipindi cha miaka 12 kumefanyika
uchunguzi wa visa 9 vyote vinavyodaiwa
barani Afrika, na hadi sasa ina
watuhumiwa 7 walio kizuizini. 

13 wangali
wakisakwa licha ya waranti uliotolewa.
Miongoni mwao ni Rais wa Sudan Omar
Hassan al-Bashir na Kiongozi wa waasi wa kundi la Lord's Resistance Army (LRA) nchini Uganda, Joseph Kony.

Wapalestina kukubaliwa rasmi
uwanachama wa ICC
Wakati huo huo, Wapalestina
wamekubaliwa rasmi kuwa waangalizi
katika mkutano wa kilele wa nchi 122 za
ICC. Mahakama hiyo inasema uamuzi huo
ni hatua moja mbele ya kujiunga kama
mwanachama kamili wa mahaka hiyo ya
uhalifu ya kimataifa. Rais wa Palestina
Mahmoud Abbas ametishia kuomba
uwanachama kamili ili kushinikiza
mashtaka ya uhalifu wa kivita dhidi ya
Israel.

Mkutano huo wa nchi wanachama 122 wa mahakama ya uhalifu ya kimataifa mjini New York, utadumu kwa muda wa wiki mbili.

Mwandishi: Mohammed Abdul-Rahman,
AP
chanzo DW
Mhariri: Saumu Yusuf

Chapisha Maoni

 
Top