0
Kiongozi wa mashitaka aliyewasilisha kesi ya rufaa dhidi ya Pistorius 

Mahakama nchini Afrika Kusini imemruhusu kiongozi wa mashitaka kukata rufaa dhidi ya kosa alilopatikana nalo hatia Oscar Pistorius la kumuua
mpenzi wake Reeva Steenkamp.
Kesi hio, sasa itaanza kusikiliza katika mahakama ya juu zaidi upande wa mashitaka ukitaka Pistorius
ahukumiwe kwa kumuua mpenzi wake kwa kusudi.

Jaji Thokozile Masipa, alisema hataruhusu rufaa dhidi ya hukumu iliyotolewa ya miaka mitano dhidi
ya Oscar mwezi Oktoba.
Kiongozi wa mashitaka Gerrie Nel aliambia mahakama kuwa hukumu hio ni ndogo sana ikilinganishwa na kosa la Oscar.

Chapisha Maoni

 
Top