Kijana ambaye jina lake haikufahamika mara moja, amenusurika kuuawa na wananchi wenye hasira kwa tuhuma za wizi wa pikipiki jijini Dar.
Tukio hilo la kusisimua limetokea jana asubuhi Magomeni-Mwembechai, ambapo lilisababisha foleni ndefu ya magari wakati kijana huyo akiadhibiwa na wananchi.
Mashuhuda wa tukio hili walisema kijana huyo na wenzake waliiba pikipiki mbali na hapo Mwembechai ila katika purukushani na wamiliki wa chombo kile, kijana yule alijikuta akianguka
kutoka kwenye pikipiki eneo lile na kuzingirwa na waendesha pikipiki wa pale wanaojulikana kama ‘bodaboda’ walioanza kumshushia kipigo baada
ya mmiliki wa pikipiki husika aliyekuwa
akiwafukuza kusema kijana huyo alikuwa na wenzake waliokimbia na chombo hicho.
Pamoja na kipigo alichopewa, wananchi waliamua kumvisha tairi shingoni wakiwa tayari kumchoma moto ambapo dakika chache tu baadaye askari
walifika na kumwokoa.
Kijana huyo aliyekuwa bado hai, aliokolewa naaskari wa doria waliomchukua pamoja na mtu
aliyejitaja kama mmiliki wa pikipiki iliyoibiwa.

Chapisha Maoni