0
KIongozi wa Oparesheni wa kundi la Al Qaeda
auawa nchini Pakistan katika uvamizi.


Kiongozi mwandamizi wa kundi la wanamgambo wa Al Qaeda anayeshukiwa kupanga kulipuwa treni
mijini New York na London ameuawa nchini Pakistan,kwa mujibu wa Jeshi la nchi hiyo.

Adnan el Shukrijumah aliuawa katika shambulizi kazkazini magharibi mwa Pakistan karibu na mpaka wa Afghanistan,jeshi hilo limesema.

Maafisa wa kundi la Ujasusi kutoka Marekani FBI wamekuwa wakimtaja kuwa mkuu wa kitengo cha oparesheni katika kundi la Al Qaeda,wadhfa ambao
ulishikiliwa na mtu anayeshukiwa kupanga njama za shambulizi la Septemba 11 Khalid Sheikh
Mohammed.

Shukrijumah alizaliwa nchini Saudi Arabia na kuishi kwa miaka kadhaa nchini Marekani.

Aliorodheshwa katika mashtaka kama muhusika wa Kupanga njama katika kesi dhidi ya watu watatu wanaoshutumiwa kwa kupanga mashambulizi ya
kujitolea muhanga katika barabara za treni mjini New York mwaka 2009.

Pia anashukiwa kupanga njama za kutekeleza mashambulizi ya kundi ya Al Qaeda nchini Panama,Norway na Uingereza.

Uvamizi huo wa mapema leo ulifanyika katika jimbo la Shinwarsak kusini mwa Waziristan,ambalo ni eneo la Kazkazini magharibi mwa mkoa uliopo
karibu na mpaka.

Jimbo hilo ni kambi ya wapiganaji wa Taliban nchini Pakistan na washirika wao.

Chapisha Maoni

 
Top