0
KOCHA wa Yanga, Mbrazil Marcio
Maximo amewaaga rasmi leo asubuhi
wachezaji wa timu hiyo kwenye mazoezi
uwanja wa Sekondari ya Loyola huku
akitarajia kuvuna zaidi ya Milioni 20
ndani ya klabu hiyo ikiwa ni mshahara
wake wa dola 1200 na yupo kwenye
harakati za kudai fidia ya kuvunjiwa
mkataba na kuletwa mrithi wake kabla
uongozi wa klabu hiyo haujamaliza nae.

Hata hivyo, tayari Maximo ameaga
wachezaji wake kwenye mazoezi ya
asubuhi leo ambapo mazoezi hayo
yaligeuka shubiri baada ya Maximo
kuwakusanya wachezaji wake na
kuwambia kuwa kuanzia leo sio kocha
wa timu hiyo tena na kuwatakia maisha
mema ndani ya klabu hiyo ya Jangwani.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti
wachezaji wa klabu hiyo ambao pia
hawajaridhishwa na uamuzi wa uongozi wa klabu hiyo kumuacha mshambuliaji Hamis Kiiza na kumsajili Amis Tambwe.

Mmoja wa wachezaji hao alisema "Ni kweli kocha ametuaga asubuhi daa! ndio hivyo tumesikitika lakini hatuna jinsi."
Naye mchezaji mwingine ambaye hakutaka jina lake litajwe alisema "Inaumiza sana jana (juzi) tumefanya nae mazoezi vizuri kabisa tena amechangamka kama kawaida
kumbe nyuma kuna mambo yanaendelea, leo asubuhi tumeenda mazoezi kama kawaida tukijua tunafanya mazoezi matokeo yake
anasema acheni kila kitu kaeni hapo nataka kuzungumza na nyinyi.

"Uwezi kuamini kidogo machozi yanitoke pale aliposema kuanzia leo yeye sio kocha wetu tena, dah inaumiza sana, mtu ambaye mmemzoea mnafanya nae kazi kuondoka,
ndo hivyo wakubwa wemeshaamua bwana wenye timu yao.

Wakati huyo akisema hayo, mchezaji nguli wa timu hiyo yeye alisema "Hakuna
mchezaji kwa kweli aliyependezwa na
kitendo cha uongozi, yani kwenye mazoezi asubuhi ilikuwa kama msiba, 'mood' ya kufanya mazoezi iilisha kabisa, yani hakuna aliyekuwa na hamu ya kuendelea na mazoezi.

"Tumefanya kidogo mazoezi tukaondoka, ukiangalia ni sawa tumefungwa cha muhimu ilikuwa ni kukaa chini na kuzungumza na kuangalia cha kufanya, kama kuna mapungufu basi yafanyiwe kazi,
mimi sijaona haja ya kumfukuza kocha hasa kipindi kama hichi."

Meneja wa timu hiyo Hafidhi Saleh alikiri
Maximo kuaga wachezaji kabla ya mazoezi ya timu hiyo kuanza akiwapa moyo wajitume kwa kuwa ni wachezaji wazuri na timu ni nzuri na kuwataka kuongeza bidii ili wafike mbali.

"Kwa kweli inasikitisha hakuna mchezaji
wala mtu aliyefurahia, kama yupo labda
kimoyomoyo ila dah imetuumiza, ni mazoea cha muhimu tugange yajayo hayo mengine tuwaachie viongozi."alisema Saleh Saleh alisema kuwa tayari kocha Hans van
Der Pluijm ambaye amefikia kwenye hoteli ya Tansoma jana alikuwa kwenye mazungumzo na uongozi wa klabu hiyo ili aichukue nafasi ya mbrazil Marcio Maximo ambaye amekumbwa na kipunga cha kutimuliwa baada ya kunyukwa mabao 2-0 katika mechi
ya mtani Jembe, akiwa ni kocha wa pili
kutimuliwa Yanga baada ya matokeo ya
mtani jembe mwaka jana alitimuliwa Ernie Brandts baada ya kunyukwa mabao 3-1 na nafasi yake kuchukuliwa na Pluijim ambaye nae hakukaa sana akaikacha timu hiyo baada ya kupata kibara nchini Saudi Arabia.

Wakati huo huo, uongozi wa Yanga
umegwaya mchezaji Andry Countinouh
kuvunja mkataba wake baada ya kuwa
wangelazimika kuvunja kibubu cha Sh185 milioni ili kumlipa fidia ya mshahara wake ambao ni dola 2800 kwa mwezi.

Katika hatua nyingine, pamoja na Yanga
kumfungashia virago Emerson De Oliveira Neves Roque imemuombea kibali cha usajili wa kimataifa (ITC) kutoka Bonsucesso Brasil
kwenda Yanga.

Mkurugenzi wa mashindano ya TFF,
Boniface Wambura alisema kuwa TFF haina taarifa za Yanga kumuacha mbrazili huyo.

Chapisha Maoni

 
Top