Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza, Halifa Hida, ofisini kwake akiwa mbele ya waandishi wa habari ametangaza matokeo ya uchaguzi wawenyeviti wa serikali za mitaa katika
mitaa 175 ya Jimbo la Nyamagana jijini Mwanza.
Hida amesema katika kata ya Mabatini yenye jumla ya mitaa 6, CCM 5 Chadema 1, kata ya Mbugani yenye mitaa 6, CCM 3 Chadema 3,
kata ya Butimba jumla mitaa 8, CCM mitaa 3 Chadema 5,
kata ya Luchelele mitaa 10, CCM 4 na Chadema 5, kata ya Mirongo mitaa 3, CCM 2 CUF 1, kata ya Nyegezi mitaa 8, CCM 2 Chadema 6,
kata ya Mkuyuni mitaa 8, CCM 3 Chadema 3 na CUF 2.
Kata nyingine ni kata ya Lwanhima mitaa 18, CCM 16 Chadema 2, kata ya Buhongwa mitaa18, CCM 14 Chadema 4,
kata ya Nyamagana mitaa 4, CCM
2 Chadema2, kata ya Mkolani mitaa 10, CCM 5 Chadema 5, kata ya Igogo mitaa 9, CCM 4 Chadema 1 na CUF 4, kata ya Pamba mitaa 10, CCM 7 Chadema 3,
Kata ya Igoma mitaa 14, CCM 7 Chdema 6 na ACT 1, kata ya Kishiri 12, CCM 6
na Chadema 6.
Katika Kata ya Mahina jumla ya mitaa 9, CCM 4 na Chadema 5, Kata ya Mhandu mitaa 11, CCM 6 na Chadema 5,
Kata ya Isamilo mitaa 11, CCM 3 na Chadema 8 ambapo jumla CCM imeshinda mitaa 96 sawa na asilimia 54.86%, Chadema kimepata mitaa 70 sawa na asilimia 40%, CUF kimepata mitaa 7 sawa na aslimia 4.00% na ACT kimepata mtaa 1 sawa na aslimia 0.56% ya mitaa yote 175.
ILEMELA
Nako wilayani Ilemela Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Wilaya ya Ilemela Jastine Lukaza ametangaza matokeo ya mitaa yote 168, CCM
ikipata Mitaa 106 sawa na asilimia 63 na
CHADEMA imepata Mitaa 62 sawa na asilimia 37.
MISUNGWI
Vijiji - CCM imeshinda vijiji 98, CHADEMA 15, Vitongoji CCM 508, CHADEMA 150.
UKEREWE
Vijiji - CCM 28, CHADEMA 47, Vitongoji CCM 311, CHADEMA 194
SENGEREMA
Mjini - CCM mitaa 7, CHADEMA 14.
Chapisha Maoni