0
Kumetokea hali isiyo ya kawaida iliyowastua wananchi wa mtaa wa Msalala Road mkoani Geita
ya kuondokewa na mgombea wa nafasi ya Wajumbe wa Serikali za Mitaa (Viti Maalumu) kupitia chama cha Demokrasia na Maendeleo
(CHADEMA) Bertha Nchimanyi (40) baada ya kukutwa amekufa kisimani.

Tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia jana majira ya saa 9:00 wakati mgombea huyo alipotoka nje kuongea na simu yake ya mkononi Inaelezwa kuwa marehemu alikuwa akisimamia
zoezi la kuhesabu kura zake,na wakati zoezi hilo likiendelea alitoka nje kuongea na simu na hakurudi tena.

"Martha nilikuwa naye ilipofika majira ya saa 9 usiku wakati tunahesabu kura, aliniambia anatoka mara moja nje lakini hakurudi tena," aliiambia Africa Newss, mgombea wa nafasi ya uenyekiti kupitia CHADEMA, Elineema Mafie.
 Naye wakala wa mgombea huyo Maselina Simbasana ambaye alisaini matokeo ya marehemu huyo baada ya kuonekana hayupo, alisema marehemu alikuwa na mtoto mdogo hivyo walivyomtafuta walidhani huenda alikwenda nyumbani kunyonyesha mtoto wake.

Kamanda wa jeshi la polisi Mkoa wa Geita Joseph Konyo alithibitisha kuwepo kwa tukio hilo na kusema kwamba, jeshi linaendelea na uchunguzi wa kina ili kubaini chazo cha tukio.

“Ni kweli kuna tukio la mgombea wa chadema kutumbukia kisimani, kwa taarifa tulizonazo inaelezwa alitoka nje kuongea na simu wakati anaongea hakujua kama kuna kisima kirefu eneo
alilokuwepo, alitumbukia na kufariki dunia”. Katibu wa Chadema Jimbo la Geita Mutta Robert alisema kuwa kifo cha mgombea huyo ni Mapenzi ya Mungu .

“Mgombea wetu ameondoka na alikuwa
ameshinda ,alikuwa mchapakazi
mzuri ,tulimpenda zaidi lakini Mungu amempendavzaidi na yote tunamwachia yeye” alisema Robert.

Chapisha Maoni

 
Top