0
Ikulu imesema pamoja na kuwa Rais Jakaya Kikwete amekwishapokea maazimio ya Bunge kuhusu wanaotuhumiwa kuchota Sh306 bilioni
katika Akaunti ya Tegeta Escrow, hawezi
kuwachukulia hatua mpaka hapo uchunguzi kuhusu suala hilo utakapokamilika.

“Rais lazima aagize vyombo vya uchunguzi kufanya kazi yake na baada ya hapo ndipo atapata mahali pa kuanzia. Watu wengi walitaka Rais
Kikwete achukue hatua baada ya kupewa maazimio ya Bunge. Jambo hilo haliwezekani,” Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue alisema jana na kuongeza kuwa hatua
zitachukuliwa kwa watakaobainika kuwa na makosa ya kimaadili au jinai baada ya uchunguzi.

Alisema uchunguzi kuhusu uchotwaji wa mabilioni hayo uliofanywa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) pamoja na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) pia
utazingatiwa na Rais katika kutoa uamuzi.

“Maazimio ya Bunge ni mazuri ila inatakiwa muda kwanza ili Rais naye apate taarifa za uchunguzi
zaidi. Maazimio hayo ni muhimu na si ya
kupuuzwa hata kidogo,” alisema.
Alisema vyombo vinavyofanya uchunguzi kuhusu suala hilo ni vile ambavyo vilitajwa kufanya hivyo
katika maazimio manane ya Bunge.

Bavicha wamtaka Kikwete achukue hatua Baraza la Vijana wa Chadema (Bavicha), limemtaka Rais Kikwete kuacha kuhamisha wakuu wa mikoa na badala yake atoe uamuzi wa
kuwashughulisha watuhumiwa wote waliohusika na kashfa ya escrow.

Akizungumza Dar es Salaam jana, Katibu wa Bavicha, Mwita Julius alisema: “Wakati huu si mzuri wa kuanza kuhamisha wakuu wa mikoa kwa
kuwa ni gharama, ni muda wa kuwachukulia hatua wahusika wote waliotajwa bungeni wakihusika na
sakata la escrow.”

Alisema Rais anatakiwa kuwashughulikia wateule wake wote waliotajwa bungeni kwani wananchi
wanasubiri kuona mabadiliko hayo kwa haraka.
Juzi, Rais Kikwete aliteua mkuu mmoja wa mkoa na kuwahamisha wengine sita.

Chapisha Maoni

 
Top