MWANADADA anayefanya vizuri katika muziki wa kizazi kipya nchini, Judith Wambura 'Lady Jaydee' amesema kamwe hatarajii kujiingiza katika masula
ya siasa kama wanavyofanya wanamuziki wenzake.
Kauli hiyo aliitoa wakati akizungumza na
waandishi wa habari wa gazeti la Jambo Leo Dar es Salaam jana, baada ya kutembelea chumba cha habari cha gazeti hilo katika Jengo la Hifadhi
House katika makutano ya Barabara za Azikiwe na Samora.
"Binafsi sitarajii kuingia katika masula ya siasa mimi nitaendelea na muziki na hao wenzangu waliojiingiza katika siasa ni utashi wao."
Alisema anafurahi kufanya muziki na wala hajuti kwa kuwa unamuongezea kipato,kikubwa ni kutunga nyimbo zenye maudhui na mvuto na kwa
wakati husika.
Baadhi ya wanamuziki waliojiingiza katika siasa ni Joseph Mbilinyi 'Sugu' ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini kupitia Chama cha
Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Joseph Haule 'Profesa J, Khadija Shabani 'Keisha' Ummy Wenslaus 'Dokii, na wengine kama Fullgence 'Mwanacotide' ambaye yupo Chadema.
Chapisha Maoni