Inaarifiwa kuwa watu kama 30 waliuwawa katika mashambulio kwenye vijiji mashariki mwa Jamhuri ya Demokrasi ya Congo.
Inaarifiwa kuwa mashambulio hayo yalifanywa Jumamosi usiku kwenye vijiji karibu na mji wa Beni ambako watu zaidi ya 250 wameuwawa tangu mwezi Oktoba.
Wakuu na mashirika ya raia yanawalaumu wapiganaji kutoka Uganda wa kundi la ADF, lakini
baadhi ya wadadisi wanasema hakuna ushahidi wa kutosha wa kuhusisha kundi hilo.
chanzo: BBC
Chapisha Maoni