0
 Kampeni za uchaguzi wa Serikali za Mitaa, ambazo zimekuwa zikitawaliwa na zomeazomea na vurugu, zimechukua sura mpya baada ya wafuasi wa CCM kuitwa ‘escrow’ kiasi cha katibu wa chama hicho wilayani Arusha, Feruz Bana kutaka wapinzani wazungumze hoja.

CCM ilijikuta kwenye kashfa hiyo inayohusu uchotwaji wa fedha kutoka Akaunti ya Tegeta Escrow iliyofunguliwa Benki Kuu ya Tanzania, baada ya mawaziri watatu, mmoja wa zamani,
mwanasheria mkuu wa sasa na wa zamani kuhusishwa kwa njia moja au nyingine.

Bana amewataka wafuasi wa Chadema, kujadili kitu watakachowafanyia wakazi wa Arusha iwapo watashinda badala ya kung’ang’ania hoja moja ya wizi wa fedha za escrow.

Bana alikerwa na hayo jana akieleza
anashangazwa na wafuasi wa CCM kuwaitwa escrow wakati hoja hiyo ilikuwa ya Bunge zima.

“Walete hoja siyo ushabiki, mikutano yao hoja kubwa imekuwa ni wizi wa fedha za escrow,” alisema.

Chapisha Maoni

 
Top