Staa mwenye shepu ya aina yake ndani ya Bongo Movies, Tamrina Poshi ‘Amanda’ ameibuka na kusema kuwa siku ikifika atarejea kwa Mwenyezi
Mungu lakini kwa sasa bado anakula ujana.
Akiongea na Gazeti la Ijumaa Wikienda, Amanda alisema kwa sasa umri wake unamruhusu kula ujana kwa mambo ya starehe kama kuvaa mavazi ya kuacha mwili wake nusu utupu kwa sababu
muda wa kurejea kwa Mungu bado haujafika.
“Jamani niacheni na mavazi yangu, ukifika muda nitarejea naona mnanisema sana, kama wewe
Mungu amekujalia kusali, mshukuru mimi muda huo bado haujafika,” alisema Amanda ambaye wakati huo alikuwa ametupia kivazi kilichomuacha
wazi sehemu kubwa ya mwili wake hasa tumboni.
Chapisha Maoni