STAA wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul 'Diamond Platnumz' usiku wa kuamkia leo ameshinda tuzo nyingine huko Lagos nchini Nigeria kutoka The Future Awards Africa Prize in Entertainment 2014.
Tuzo hiyo ya Diamond ilipokelewa na Meneja wake Salaam na kwenye kipengele cha tuzo hiyo kulikuwa na wakali wengine wakiwemo Panshack
au Ice Prince wa Nigeria na Michael Kwesi kutoka nchini Ghana.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Diamond aliandika ujumbe huu: "Thanks God, we have cheated another one on the future Awards Africa in Lagos Nigeria…#Samenight Thank You Allah"
Chapisha Maoni