0
MANCHESTER City imetoka nyuma na kushinda mabao 4-1 dhidi ya wenyeji Sunderland Uwanja wa Light usiku huu katika mchezo wa Ligi Kuu ya England.

Connor Wickham alimaliia krosi nzuri ya
Sebastian Larsson kuifungia bao la kuongoza Sunderland dakika ya 19, kabla ya Sergio Aguero kuisawazishia Manchester City dakika ya 21.

Bao hilo la Aguero lilikuwa bao la kwanza kwa Manchester City kufunga Uwanja wa Light tangu Machi mwaka 2010, wakati Stevan Jovetic aliifungia bao la pili City dakika ya 39.

Pablo Zabaleta akaifungia timu ya Manuel Pellegrini bao la tatu, kabla ya Aguero kufunga la nne.

Chapisha Maoni

 
Top