Mtoto mwenye umri wa mwaka mmoja mkazi wa kijiji cha Kindo wilaya ya Mvomero mkoani Morogoro amefariki dunia baada ya kunyongwa na baba yake wa kambo kufuatia migogoro ya
kifamilia kati yake na mkewe.
Kamanda wa polisi mkoa wa Morogoro Leonard Paul amesema mtoto Abdallah Hamis amenyongwa na baba yake wa kambo Zamili Shabani (27) muda mfupi baada ya mama wa mtoto kwenda dukani kununua mahitaji na aliporejea aliingia chumbani kumwamsha mtoto
ndipo akagundua kuwa mtoto amekufa ambapo mtuhumiwa kwa wasiwasi alianza kukimbia na mama huyo alipiga kelele ya kuomba msaada kwa
majirani hadi alipokamatwa.
Katika hatua nyingine jeshi la polisi mkoa wa Morogoro linamshikilia mtuhumiwa mmoja Abadalla Kifungo (40) mkazi wa Malola wilaya ya
Ulanga mkoani Morogoro kwa tuhuma za kukutwa na silaha aina ya Shortgun na risasi mbili ambapo inasadikiwa kuwa alikuwa akijihusisha na matukio
ya ujangili ambapo watuhumiwa hao wa matukio mawili tofauti watafikishwa mahakamani kujibu mashtaka.
Chapisha Maoni