
Ushindi huo, unaipeleka United nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi Kuu England kwa kutimiza pointi 31, ikizidiwa tano na Manchester City walio nafasi ya pili.
Nahodha wa Mashetani hao Wekundu, Wayne Rooney alifunga sherehe za mabao dakika ya 12 akimalizia kazi nzuri ya winga Antonio Valencia aliyewatoka mabeki wa Liverpool.
Rooney alifunga bao hilo kiasi cha sekunde 25 baada ya Raheem Sterling kukosa bao la wazi upande wa Liverpool, kabla ya Juan Mata kufunga la pili dakika ya 40 akimalizia kazi ya Robin van Persie.
Mshambuliaji wa Uholanzi, Van Persie
akahitimisha ushindi wa timu ya Louis Van Gaal
kwa bao la tatu dakika ya 71 akimalizia pasi ya
Mata.

Liverpool; Jones, Skrtel, Johnson/Toure dk25, Lovren, Moreno/Markovic dk68, Henderson, Allen, Gerrard, Coutinho, Lallana/Balotelli dk46 na Sterling.


Chapisha Maoni
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.