Wakazi wa Mtaa wa Migombani, Uliopo
Katika kata ya Segerea Manispaa ya Ilala
Jijini Dar Es Salaam wakiwa wamelizunguka
gari la Afisa Mtendaji wa Kata ya Segerea aliyefika majira ya saa tisa kamili mchana huu na kutangaza kusitisha uchaguzi wa
serikali ya mitaa kimya kimya.
Afisa Mtendaji wa Kata ya Segerea (katikati mwenye shati la draft) akiwa kawekwa mtukati mara baada ya kuja na kutaka kusitisha uchaguzi bila sababu ya msingi.
waliomzunguka ni wakazi wa mtaa wa
segerea wakimuhoji afisa mtendaji huyo
sababu ya kutaka kusitisha uchaguzi huo wakati hakukuwa na vurugu wala kero ya aina yoyote iliyojitokeza katika kituo cha kupigia kura cha Migombani.
Wakazi wa Mtaa wa migombani wakumzuia afisa mtendaji kuondoka hadi pale atakapotangaza tena kuwa uchaguzi unaendelea
Msimamizi wa Uchaguzi wa serikali ya Mtaa wa Migombani katika Kituo cha uchaguzi wa Migomabni akielezea sababu za
kusimamisha uchaguzi huo kwa muda
kutokana na kusubilia barua ya kumtaka
kuendelea na uchaguzi kutoka kwa afisa
mtendaji wa Kata ya Segerea aliyetaka
kujaribu kusitisha Uchaguzi huo kwa
kisingizio cha Kutumwa na Mkurugenzi wa Uchaguzi.
Afisa Mtendaji wa Kata ya Segerea,
Akiandika barua ya kutamka kuwa uchaguzi unaendelea mara baada ya wakazi wa mtaa wa migombani kutaka afisa huyo kueleza sababu za msingi za kutaka kujaribu kusitisha uchaguzi huo.Pembeni ni wakazi
wa Mtaa wa Migombani wakishuhudia kuwa afisa mtendaji huyo anaandika ipasavyo hiyo barua.
Hali ya Kushtusha imetokea katika
uchaguzi wa Serikali ya Mtaa wa
Migombani Mara baada ya Afisa Mtendaji
huyo kuja na kutangaza kimyakimya
Kuwa UChaguzi huo umesitishwa, Mara
baada ya wakazi wa mtaa wa migombani
kusikia ndipo walipoanza sasa kutafuta
mchawi na kumtia nguvuni afisa
mtendaji huyo wa mtaa kwa kutaka
kujua sababu za msingi zinazopelekea
yeye kuja kutangaza kusitisha uchaguzi
huo.
Afisa mtendaji huyo baada ya kuulizwa
sababu za msingi alijitetea kuwa
ameagizwa na Mkurungenzi wa Uchaguzi wa Manispaa ya ilala.
Mara baada ya Kutoa sababu hiyo ndipo wakazi wa mtaa wa migombani walipoona kuna dalili za
kuchakachuliwa kwa kura zao ndipo
walipomuweka mtu kati na kumtaka
Afisa mtendaji huyo kutangaza kwa
maandishi kuwa uchaguzi unaendelea
ndipo wakazi hao walipomuweka mtu
kati na kuhakikisha anaandika barua hiyo ya kutaka kuendelea na uchaguzi.
kuchakachuliwa kwa kura zao ndipo
walipomuweka mtu kati na kumtaka
Afisa mtendaji huyo kutangaza kwa
maandishi kuwa uchaguzi unaendelea
ndipo wakazi hao walipomuweka mtu
kati na kuhakikisha anaandika barua hiyo ya kutaka kuendelea na uchaguzi.
Chapisha Maoni