Mgombea wa nafasi ya Mwenyekiti wa Mtaa wa Migombani Kupitia tiketi ya Chama cha Demokrasi na Maendeleo (Chadema) Japhet Kembo akifurahia huku akipongezwa na wanachama na wapenzi wa Chadema mara baada ya kuibuka mshindi wa Kiti chaMwenyekiti kwa Kupata Kura 510 huku CCM wakiwa wamepata kura 215 na NCCR kupata kura 205
Mawakala wa wagombea wa nafasi yaMwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa
Migombani wakihesabu kura ambapo
sanduku hilo ndio lilikuwa sanduku la
mwisho kuhesabiwa katika Kituo cha
Kupigia kura cha Migombani ambao wakazi wa Mtaa wa Migombani walikuwa wakisubiria matokeo
Askari Polisi wakiwa katika kituo chaKupigia Kura cha Migombani kwaajili ya
kuimarisha ulinzi na mpaka zoezi la
kuhesabu kura likimalizika kwa Mgombea wa Chadema kuibuka Mshindi hakuna fujo zilizotokea.
Baadhi ya wakazi wa Mtaa wa Migombani Wakisubiria Matokeo ya Uchaguzi wa Serikali ya Mtaa wa Migombani ambapo mpaka matokeo yanatangazwa Chadema iliibuka na Kura 510, CCM ikiwa imepata kura 215 na NCCR wakiwa na kura 205.
Baadhi ya wapita njia nao ilibidi wasimame maana uchaguzi huu ulivuta hisia za watu wengi kutokana na hali iliyoonyeshwa na wakazi wa mtaa huo kukaa mpaka dakika za mwisho
Chapisha Maoni