0
MANCHESTER United imeendelea kufanya vizuri katika Ligi Kuu ya England kufuatia ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Newcastle Uwanja wa Old
Trafford.

Ilikuwa ni siku nzuri kwa Nahodha Wayne Rooney, aliyeifungia Manchester United mabao mawili na kutoa pasi ya bao moja, la tatu.

Rooney alifunga bao la kwanza kwa pasi ya Radamel Falcao dakika ya 23 katika shambulizi alilolianzisha mwenyewe kutokea nyuma, kabla ya kufunga la pili dakika 13 baadaye kwa pasi
la Juan Mata.

Nahodha huyo wa England pia, akampasia mpira mzuri Robin van Persie kufunga bao la tatu kwa kichwa dakika ya 53, kabla ya Papis
Cisse kuifungia bao la kufutia machozi
Newcastle kwa penalti dakika ya 87.

Kwa ushindi huo, Mashetani Wekundu
wanaendelea kukamata nafasi ya tatu kwenye msimamo wa Ligi Kuu, wakizidiwa pointi 10 na vinara, Chelsea.

Kikosi cha Manchester United kilikuwa; De Gea, Jones, McNair, Evans, Valencia/Rafael dk80, Rooney, Carrick/Fletcher dk62, Young, Mata, Falcao/Wilson dk65 na Van Persie.

Newcastle: Alnwick, Janmaat, Steven Taylor, Coloccini, Dummett/Cabella dk63, Anita, Colback, Armstrong/Cisse dk63, Sissoko, Gouffran na Perez/Vuckic dk82.

Chapisha Maoni

 
Top