0

Klabu ya Simba imekubali kumuuzia Mohammed
Dewji asilimia 51 ya hisa za klabu naye ameahidi
kufanya makubwa pamoja na ujenzi wa uwanja
Kamati ya Utendaji ya klabu ya Simba na
Mohamed Dewji imefikia muafaka wa kuiingiza
klabu hiyo katika uendeshwaji wa mfumo wa hisa
kufuatia kikao cha pande zote mbili kilichofanyika
jana Dar es Salaam.
Msemaji wa klabu ya Simba Hajji Manara
ameiambia Goal , kikao hicho kimefanyika kwa
mafanikio makubwa na kufikia maamuzi hayo
ambayo anaamini ndio maamuzi ya wana Simba
wengi.
Manara amesema katika kikao cha jana, Dewji
aliwaeleza rasmi Wajumbe wa Kamati ya Utendaji
ya Simba dhamira yake ya kununua asilimia 51
ya hisa za klabu kwa Sh. Bilioni 20.
Rais huyo wa Kampuni ya Mohamed Enterprises
Limited (MeTL) baada ya kuuziwa asilimia 51 ya
hisa za Simba kwa Sh. Bilioni 20, ameahidi naye
atawawezesha wanachama wa muda mrefu wa
klabu hiyo kupewa hisa bure, ambazo wataamua
wenyewe kuuza, au kununua hisa zaidi.
Anataka kuitoa klabu kwenye Bajeti ya Bilioni 1.2
kwa mwaka hadi Bilioni 5.5 na kwa kuamini
mashabiki wa Simba wanahitaji mafanikio ya
haraka, ameahidi kusajili vizuri, kuajiri kocha
mzuri, ambavyo vyote vinaweza kugharimu Sh.
Bilioni 4 na kwamba Bilioni 1.5 itakayobaki,
ataiweka katika mradi wa ujenzi wa Uwanja.



Like Page ya Facebook Africa Newss Sports Posted: ⚽ Africa News Sports2

Chapisha Maoni

 
Top