0

Riyad Mahrez kiungo mshambuliaji wa Leicester
City kwa mara ya kwanza amebainisha kuwa
anaweza kuondoka klabu hiyo kama atapata ofa ya
maana.
Mahrez (25) mchezaji wa Kimataifa wa Algeria
amesema kuwa ingawa akili yake yote ni
kuitumikia timu yake ya Leicester msimu huu, hata
hivyo anaweza kuondoka klabuni hapo kama
atahitajika na timu kubwa zaidi.
Baada ya Arsenal kukana kutaka kumsajili, kuna
taarifa kuwa Mahrez anawindwa na FC Barcelona
huku pia Real Madrid ikidaiwa kutaka kumnyakua.
Claudio Ranieri, Meneja wa Leicester mapema
mwezi Julai aliwatahadharisha wachezaji wake
muhimu kuwa wasiondoke klabuni hapo kwani
wataujutia uamuzi huo.
Alisema huko wanakokwenda wanaweza wsipate
nafasi ya kucheza kama ilivyo kwa Leicester.
Tayari Ng'olo Kante keshatimkia Chelsea, nusura
Vardy ajiunge na Arsenal kabla ya kuanza kwa
michuano ya Euro 2016.



Like Page ya Facebook Africa Newss Sports Posted: ⚽ Africa News Sports2

Chapisha Maoni

 
Top