Ni muujiza pekee utakaoifanya Manchester City
ishindwe kuingia hatua ya makundi ligi ya
mabingwa Ulaya baada ya jana kupata ushindi
mnono ugenini kwa kuwalaza Steaua Bucharest
mabao 5-0.
Sergio Aguero ndio alikuwa muuaji wa Bucharest
baada ya kufunga mabao matatu 'hat-trik' huku pia
akikosa mikwaju miwili ya penati.
David Silver na Diego Milito nao pia walizifumania
nyavu kukamilisha idadi ya mabao hayo matano
katika mchezo uliokuwa wa upande mmoja.
Mchezo wa marudiano utapigwa Agosti 24 kwenye
dimba la Etihad, Manchester City ikitarajiwa
kutinga hatua ya makundi.
Like Page ya Facebook Africa Newss Sports Posted: ⚽ Africa News Sports2
Chapisha Maoni