0
Rais wa Nigeria Goodluck Jonathan amethibitisha rasmi kuwa atagombea tena kiti hicho mwaka ujao.

Katika sherehe ya kufana katika mji mkuu Abuja, Bwana Jonathan alimwagiwa sifa na wafuasi wa
chama chake, kabla ya kujitangaza kama mgombea.

Amekuwa rais wa taifa hilo maaruifu barani Afrika tangu mwaka 2010.
Waandishi wa habari wanasema uchaguzi wake utakuwa mkali hususan kama upinzani utaungana
dhidi ya mtu mmoja.

Mbali na siasa , eneo la Kaskazini Mashariki ya Nigeria, linaendelea kukumbwa na vurugu huku
Boko Haram wakiwa tu ndio wameteka mji mwingine wa Mahia na kujiongezea idadi ya miji wanayodhibiti.

Rais Jonathan alitoa wito wa kimya cha dakika moja kwa vijana 46 waliouawa Jumatatu katika shambulizi la kujitoa mhanga dhidi ya shule ya upili ya kuchochea zaidi hali.

Rais Jonathan amekuwa akikosolewa kwa kushindwa kushughulikia suala la wanamgambo wa Boko haram ipasavyo.
Lakini wanasiasa wa vyama vyote wanaonekana kuwa na ajenda ya kupata mamlaka zaidi kuliko kumaliza harakatai za wapiganaji wa Boko Haram ambao wamekuwa kero kwa taifa hilo.

Chapisha Maoni

 
Top