0
Watu nchini Guinea wameanza mgomo wa chakula wakipinga kuwepo kwa wanajeshi katika kijiji ambako kikundi cha maafisa wa afya waliokuwa
wanahamasisha kuhusu Ebola waliuawa mwezi Septemba.

Takriban viongozi 20 kutoka kijiji cha Wome wamepiga kambi nje ya majengo ya bunge tangu kuanza kususia chakula.
Kuwepo kwa wanajeshi katika kijiji hicho
kumewalazimisha watu 6,000 kutoroka makwao pamoja na watoto 500 kukimbilia msituni kulingana na kiongozi mmoja wa upinzani. Serikali haijatoa tamko lolote kuhusu madai hayo
sawa na jeshi.

Mnamo mwezi Septemba, serikali iliwatuhumu wanakijiji kwa kuwaua watu 8 waliokuwa wanahamasisha watu kuhusu ugonjwa hatari wa
Ebola.

Wanajeshi wa Guinea wametuhumiwa kwa kufanya vitendo vya ukiukwaji wa haki za binadamu. Baadhi ya mili ya maafisa hao wa afya ilipatikana
katika bwawa la maji taka kusini mashariki mwa mji wa Nzerekore.

Sababu ya maafisa hao kushambuliwa haijulikani ingawa lilitokea wakati jamii nyingi zilikuwa zinapinga kuwepo kwa ugonjwa huo wa Ebola au kuwatuhumu wahudumu hao kwa kusambaza virusi
Ugonjwa wa Ebola uligundulika kwanza nchini Guinea mwezi Machi kabla ya kuenea nchini Liberia na Sierra Leone.

Kiongozi wa upinzani nchini humo, aliambia BBC kuwa amejiunga na wanakijiji wanaogoma kula
ambao wako chini ya ulinzi wa jeshi.
Miongoni mwa watu waliotorokea msituni, 13 waliripotiwa kufariki kutokana na hali mbaya ya mazingira.

Chapisha Maoni

 
Top