Kipa wa Barcelona Claudio Bravo anatarajiwa
kufanya mazungumzo na Man City Alhamisi
kukamilisha uhamisho kwenda Uingereza kwa
mujibu wa habari
Manchester City imeanza mchakato wa kuisaka
saini ya kipa wa Barcelona, raia wa Chile baada
ya Pep Guardiola kuamua kumwondoa Joe Hart
kwenye nafasi ya kipa nambari moja wa klabu
hiyo.
Nyota huyo wa kimataifa wa Uingereza hakucheza
mechi ya ufunguzi Ligi Kuu Uingereza dhidi ya
Sunderland na sasa klabu imekubali kutoa kitita
cha paundi milioni 21 kumsajili Bravo.
Bosi wa Barcelona Luis Enrique hakutaka
kuzungumzia mustakabali wa kipa wake
alipoulizwa na waandishi Jumanne asubuhi.
Lakini kwa mujibu wa gazeti la Catalan, Sport,
kipa huyo mwenye umri wa miaka 33 anatarajia
kwenda Uingereza Alhamisi kukamilisha
uhamisho wake kwenda Etihad.
Barcelona inataka kubaki na Bravo, lakini shauku
ya Marc-Andre ter Stegen kutaka kuwa kipa
nambari moja imewalazimu kufikiria kumruhusu.
Katika umri wa miaka 24, Ter Stegen anaonekana
kuwa msaada wa muda mrefu na anastahili kuwa
kipa nambari moja wa Barcelona kuanzia msimu
huu na kuendelea.
Like Page ya Facebook Africa Newss Sports Posted: ⚽ Africa News Sports2
Chapisha Maoni