0

Beki wa zamani wa Liverpool, Jamie Carragher
anaamini kwamba Jurgen Klopp na Antonio
Conte wana ukaribu na wachezaji tofauti na
Arsene Wenger
Klopp wa Liverpool na Conte wa Chelsea wote
wameanza vizuri msimu mpya kwa ushindi baada
ya kuifunga Arsenal na West Ham United, na
jitihada za makocha hao zilikuwa dhahiri pande
zote.
Mjerumani Jurgen Klopp alikuwa na midadi kama
ilivyo kawaida yake, hata kumbeba mchezaji wake
mpya Sadio Mane mgongoni baada ya kufunga
goli safi sana na kufanya idadi ya magoli kuwa
4-1 dimbani Emirates.


Conte naye alichizika Diego Costa alipoifungia
Chelsea goli dakika ya 89, goli la ushindi, na
alishangilia na umati wa mashabiki uwanjani
Stamford Bridge, Bwana Carragher anaamini
ukaribu walio nao kwa wachezaji ni tofauti kubwa
sana ukilinganisha na hali ya Arsenal.


"Mimi si shabiki wa Arsenal, lakini naelewa kwa
kina sababu ya mashabiki kuwa na hasira na
jazba kali - hata kama ni mechi moja tu
waliyokosa hadi sasa," Carragher alisema.
"Kuona umati wa watu usio na utulivu -
Sikufurahia kuona idadi kubwa ya mashabiki
msimu uliopita wakiandamana na mabango na
vitu vingi nisivyovipenda, si dhidi ya Arsenal
lakini dhidi ya klabu zote. Lakini mwanzo wa kila
msimu, kila shabiki huwa na matarajio ya
mafanikio, imani na tumaini kwamba jambo fulani
litatokea."
"Lakini kwa Arsenal, mwaka hadi mwaka mambo
yanakwenda kinyume nyume, idadi ya mashabiki
inashuka, kila mmoja anavunjika moyo na hali ni
ile ile. Wamefungwa, nadhani wamekuwa
wakipoteza mechi ya kwanza misimu mitatu
iliyopita sasa. Mara ya mwisho walifungwa na
West Ham, miaka miwili iliyopita ilikuwa Astoni
Villa, na dhidi ya Liverpool sasa; na unataka
wachezaji wasio thabiti kuleta mafanikio, huku
ukifikiria hali ya Metesacker - Nadhani
watakwenda kumnunua beki kutoka Valencia -
kwa nini hilo halikufanyika miezi miwili iliyopita?
"Kuna kitu hakipo sawa kwenye kikosi, baina ya
wachezaji dimbani, na umati wa mashabiki, hata
meneja pia. Lakini kwa Klopp na Conte hali si
mbaya kulingana na umoja na ukaribu baina yao
na wachezaji.
"Kuna mgawanyiko mkubwa Arsenal, naona hali
mbaya tu kuanzia sasa hadi itakapofika mwisho
wa msimu."


Hali si nzuri Arsenal kulingana na matatizo ya
Arsene Wenger kukosa ukaribu na wachezaji,
kutosikiliza ushauri na kutojali mashabiki wake,
wachezaji wa Wenger hawashangilii hata pamoja
na kocha wao. Hii ni shida.



Like Page ya Facebook Africa Newss Sports Posted: ⚽ Africa News Sports2

Chapisha Maoni

 
Top