0

Azam FC imefuta uteja kwa Yanga, baada ya
kupoteza michezo mitatu mfululizo ya ngao ya
jamii, leo imefanikiwa kufuta uteja baada ya
kushinda kwa changamoto ya mikwaju ya penati
4-1.
Hadi dakika 90 za mpambano huo zinamalizika,
timu hizo zilitoka sare ya mabao 2-2.


Yanga iliuanza mchezo huo kwa kasi na ilikuwa ya
kwanza kupachika mabao ya kuongoza kupitia kwa
mshambuliaji wake hatari Donald Ngoma
aliyefunga mabao yote mawili kipindi cha kwanza.
Katika kipindi chote cha kwanza, Yanga ilitawala
mchezo huo huku kikosi cha Azam
kinachofundishwa na Wahispania kikishindwa
kufanya kile kilichokuwa kinatarajiwa na mashabiki
wa timu hiyo.


Hata hivyo kipindi cha pili Azam FC ilitulia hasa
dakika 15 za mwisho ambapo iliweza kusawazisha
mabao yote mawili kupitia kwa Shomari Kapombe
na Jhn Bocco 'Adebayor'.
Baada ya mpambano huo kumalizika kwa sare ya
mabao 2-2, kilichofuata ni changamoto ya mikwaju
ya penati.


Ambapo Kwa upande wa Yanga ni Deo Munish
'Dida' pekee aliyefunga mkwaju wa penati wakati
Hassan Kessy na Haruna Niyonzima walikosa.
John Bocco, Himid Mao, Kapombe na Kipre Balou
wote walifunga penati zao na hivyo Azam kutwaa
ngao ya jamii kwa ushindi wa mikwaju ya penati
4-1.
Yanga imeendelea kuwa dhaifu kwenye
changamoto za mikwaju ya penati.
Pazia la ligi kuu ya Vodacom msimu wa 2016/17
sasa limefunguliwa rasmi, Agosti 20 msimu mpya
unatarajiwa kuanza.



Like Page ya Facebook Africa Newss Sports Posted: ⚽ Africa News Sports2

Chapisha Maoni

 
Top