0

Mwanariadha wa Kenya Conseslus Kipruto
ameishindia kenya dhahabu ya nne katika mbio za
mita 3000 kuruka viunzi na maji katika michezo ya
Olimpiki inayoendelea mjini Rio.
Mwanariadha wa Marekani Even Jager alikuwa wa
pili na kujizolea medali ya fedha huku bingwa
mara mbili wa michezo ya Olimpiki Ezekiel Kemboi
akichukua nafasi ya tatu na kuishindia medali ya
shaba Kenya.
Kenya imekuwa ikijishindia medali ya dhahabu
katika mbio hiyo tangu mwaka 1994.Kenya
imejishindi medali mbili za dhahabu siku ya
Jumatano baada ya Faith Kipyegon kuibuka
mshindi katika mbio za mita 1,500 upande wa
wanawake.



Like Page ya Facebook Africa Newss Sports Posted: ⚽ Africa News Sports2

Chapisha Maoni

 
Top