Timu ya soka ya Swansea City imekataa dau la
pauni milioni 10 lilitolewa na Everton ili kuweza
kumsajili beki Ashley Williams.
Taarifa zinasema beki huyo raia wa Wales ambae
pia ni nahodha wa Swansea alikua anakaribia
kufika makubaliano ya mwisho kwenda Goodison
Park kujiunga na Everton.
Williams ambae atafikisha miaka 32 mwezi huu
anamkataba na timu yake unaomalizika mwaka
2018, msemaji wa klabu hiyo anasema hawako
tayari kumuuza beki huyo.
Beki huyo ameichezea timu yake zaidi ya michezo
300 alisajiliwa kwa kiasi cha pauni 300,000 toka
klabu ya Stockport mwaka 2008.
Everton wanasaka saini ya beki huyu ili kwenda
kuziba pengo litakaloachawa na mlinzi wao mahiri
John Stones anayehusishwa kutaka kujiunga na
matajiri wa Man City.
Posted: 👉👉 ⚽ Africa News Sports
Chapisha Maoni