0

Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), limesema kuwa
hadi sasa linamtambua Kocha wa Azam FC,
Mhispania, Zeben Hernandez, kufuatia kupokea
kibali chake cha kufanya kazi nchini huku wakiwa
hawatambui uwepo wa kocha Mcameroon, Joseph
Omog wa Simba kutokana na kibali chake
kutowasili katika shirikisho hilo.
TFF pia imezitaka klabu zote za ligi kuu
kuwasilisha nakala tatu za usajili wa kila mchezaji
ili kuweza kutambuliwa kabla ya kuupitisha usajili
huo.
Akizungumza na Championi Jumatano, Ofisa
Habari wa TFF, Alfred Lucas, amesema kabla
dirisha la usajili halijafungwa, klabu zote
zinatakiwa kuwasilisha vibali vya usajili wa
wachezaji ili vihakikiwe na iwapo kibali cha
mchezaji yeyote hakitafika, basi hatapata nafasi ya
kucheza. Alisema kwa upande wa makocha
wamepokea vya makocha wa Azam pekee.
“Tumeamua kutumia kanuni ya 67 kifungu cha 1, 2
na 8 katika kuhakikisha klabu zote za ligi kuu
zinawasilisha nakala za usajili wa wachezaji wao
ambapo zinatakiwa kuwa tatu na kila mchezaji wa
ligi kuu atalipiwa kiasi cha shilingi 50,000 na wa
Ligi Daraja la Kwanza shilingi 25,000.
“Kwa upande wa makocha, hadi leo kocha ambaye
kibali chake kimewasili hapa TFF ni wa Azam
pekee pamoja na Obrey Chirwa, mchezaji wa Yanga
na dirisha la usajili litafungwa Agosti 6, mwaka
huu.
“Upande mwingine, timu ya taifa ya vijana chini ya
miaka 17, Serengeti Boys inaelekea Afrika Kusini
kesho (leo) baada ya mechi yake na Madagascar
waliyojipima leo (jana) kwa ajili ya mchezo wake
wa Jumamosi na kisha mchezo wa marudiano
utakuwa tarehe 21 mwezi huu katika Uwanja wa
Chamazi na mwalimu ameelezea kuwa anaendelea
kuinoa safu ya ushambuliaji.
“Lakini pia kozi ya makipa wa timu za taifa na ligi
kuu imeanza Jumatatu na makipa 26 wananolewa.
Kozi inaitwa Advanced Coach, itakuwa ya siku tano
na itamalizika siku ya Ijumaa, baadhi ya makocha
wanaopata kozi hiyo ni pamoja na Mwalami
Mohamed, Juma Pondamali, Elyutery Mholery na
Salehe Ahmad wa Zanzibar Heroes,” alisema
Lucas.



Posted: 👉👉 ⚽ Africa News Sports

Chapisha Maoni

 
Top