0

SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Tanzania
(TFF) limefungua kozi ya ukocha wa
magolikipa ambapo Shirikisho la Mpira wa
Miguu Duniani (FIFA) limeipa nafasi
Tanzania kuwapa mafunzo ya juu ya
ukocha wa makipa (Advanced Goalkeeping
Coach Course) ikiandika historia kuwa nchi
ya pili barani Afrika kwa makocha wa
nafasi hiyo baada ya Botswana.
Makocha wa makipa wapatao 25 kutoka
timu za taifa, timu zinazoshiriki Ligi Kuu
ya Vodacom Tanzania Bara, wanahudhuria
kozi hiyo inayoongozwa na Alejandro
Heredia ambaye ni Mkufunzi kutoka FIFA.
Makocha hao ni Peter Manyika (Taifa Stars
ya Tanzania), Saleh Ahmed (Zanzibar
Heroes); Muharami Mohammed (Timu ya
Taifa ya Vijana wenye umri wa chini ya
miaka 17 - Serengeti Boys); Mohammed
Silima (Timu ya Taifa ya Vijana Zanzibar)
na Elyutery Mhoery (Timu ya Taifa ya
Wanawake - Twiga Stars) na msaidizi wake
ambaye pia anachezea JKT Queens, Fatuma
Omary.
Wengine ni makocha maarufu wa makipa
wakiwamo Juma Pondamali (Young
Africans); John Bosco (Majimaji ya Songea);
Salimu Tupa (Tanga); Bakari Ali Hamadi
(Wete Pemba – Zanzibar); Hafidh Muhidin
Mcha (Mkoani Pemba – Zanzibar); Mussa
Wanena (Kagera Sugar); Juma Bomba
(African Lyon), Adam Abdallah Moshi
(Simba SC), Idd Mwinchumu (Azam FC) na
Hussein Tade (Seeb Club-Oman/Toto
African). Pia wamo Khalid Adams (Mwadui
FC); Josia Steven (Mbeya City); Herry
Boymanda (Tanzania Prisons); Emmanuel
Mwansile (Polisi Morogoro); Ben Kalama
(Stand United); Abdallah Said (JKT Ruvu);
Patrick Mwangata (Mtibwa Sugar);
Augustin Malindi (Mkoa wa Kigoma);
Raphael Mpangala (Ndanda FC); Salimu
Tupa (Tanga) na nAbdul Mgude (Coastal
Union ya Tanga).
Heredia aliweza kutoa nasaha kwa
makocha hao wakati akiwanoa na kusema
kuwa “Kinachohitajika sasa ni juhudi tu.
Kozi hii haijafanyika pengine hapa barani
Afrika zaidi ya Botswana. Mjue kuwa mna
bahati na mbinu hizi mzitumie kuweza
kujenga magolikipa wziri wataoleta tija
baadae.”
Akitoa nasaha wakati wa ufunguzi wa kozi
hiyo, Makamu Rais wa TFF, Wallace Karia
aliishukuru FIFA na CAF kwa namna
inavyoshirikiana na TFF katika kuwapa
kozio nyingi za makocha wa timu kwa
wachezaji wa mbele, makocha wa makipa
na waamuzi wa madaraja tofauti. “Hakuna
kipindi TFF imepata kozi za makocha nyingi
za makocha kama kipindi hiki cha uongozi
wa Jamal Malinzi,” anasema Karia na
kuongeza: “Tumetoka kwenye kozi ya
makocha wa Daraja A sasa tuko kwenu.
Lengo ni Tanzania kuwe na makipa wazuri.
Ninyi mtaleta makipa wazuri. Na hii ni
kwa manufaa ya sasa na baadaye kwa
upende wetu, timu zetu na taifa kwa
ujumla.”
Karia aliwatia hamasa makocha hao
wanaoshiriki kozi hiyo kuwa, mara baada
ya kozi hiyo ipo siku watakwenda kuwa
wakufunzi nje ya mipaka ya nchi kadhalika
makocha ambao wanaweza kupata kazi
mahala popote duniani hasa ukizingatia
walimu wa daraja lao wako Tanzania na
Botswana tu.
Kadhalika, Makamu huyo wa Rais wa TFF
alielezea kuwa mpira wa miguu una
changamoto nyingi na nyingine
husababishwa na watalaamu hao
kubweteka kwa mafanikio. “Hili ni tatizo.
Tubadilike kifikra na kivitendo. Msilaze
damu, kuweni active (mahiri).”



Posted: 👉👉 ⚽ Africa News Sports

Chapisha Maoni

 
Top