0

Klabu ya Yanga Leo imetoa Taarifa ya kuitisha
Mkutano Mkuu wa Wanachama bila ya kufafanua
ni Ajenda yake.
Kwa mujibu wa Taarifa hiyo ambayo ilisainiwa na
Kaimu Katibu Mkuu wa Mabingwa hao wa
Tanzania Bara, Baraka Deusdedit, Mkutano huo
utafanyika Jumamosi Agosti 6 huko Bwalo la
Maafisa wa Polisi, Oyster Bay Jijini Dar es Salaam.
Taarifa hiyo pia ilibainisha kuwa Siku hiyo hiyo,
Yanga watacheza Mchezo wa Kirafiki na Mtibwa
Sugar kwenye Uwanja wa Taifa Jijini Dar es
Salaam.
Habari za hivi punde zilizozagaa zimedai Mkutano
Mkuu utafanyika Ukumbi wa Diamond Jubilee Hall
huko Upanga Jijini Dar es Salaam badala ya
Bwalo la Maafisa wa Polisi Siku hiyo hiyo
Jumamosi Agosti 6.




Posted: 👉👉 ⚽ Africa News Sports

Chapisha Maoni

 
Top