Meneja wa Juventus Massimiliano Allegri amesema
amemtaka mchezaji anayetafutwa sana na klabu
ya Manchester United Paul Pogba afike mazoezini
siku ya Jumatatu.
Mchezaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa amekuwa
likizoni Marekani baada ya kumalizika kwa
michuano ya Euro 2016.
Pogba, 23, amekuwa akihusishwa na kuhamia Old
Trafford kwa bei ya kuvunja rekodi ya dunia ya
ununuzi wa wachezaji ya pauni milioni moja.
Meneja wa United Jose Mourinho alikuwa
amedokeza kwamba klabu hiyo ilikuwa imekaribia
sana kumpata Pogba.
"Kwa sasa, Pogba ni mchezaji wa Juventus,"
amesema Allegri.
United wataanza msimu kwa mechi ya Ngao ya
Jamii dhidi ya Leicester City Jumapili.
Juventus wataanza msimu wao Serie A wiki moja
baadaye tarehe 20 Agosti.
Posted: 👉👉 ⚽ Africa News Sports
Chapisha Maoni