0
MANCHESTER United imeendeleza wimbi la ushindi katika mechi tano mfululizo za Ligi Kuu ya England baada ya usiku huu kuifunga mabao
2-1 Southampton.

United iliyokuwa ugenini, ilipata mabao yake yote kupitia kwa mshambuliaji wa kimataifa wa Uholanzi, Robin van Persie.

Bao la kwanza, van Persie alitumia makosa ya Jose Fonte dakika ya 12 kabla ya Graziano Pelle kuisawazishia Southampton dakika ya 31.

Van Persie akaifungia bao la ushindi United dakika ya 71 akiunganisha mpira wa adhabu wa Wayne Rooney na huo unakuwa ushindi wa tano mfululizo kwa Mashetani hao Wekundu katika Ligi Kuu ya England, wakati Watakatifu
wamepoteza mechi zao tatu zilizopita.

Chapisha Maoni

 
Top