MWANAMITINDO na mtangazaji mahiri
Bongo, Jokate Mwegelo amezua utata
baada ya kupiga picha akiwa ametinga
suruali iliyochanika. Akizungumzia picha
hiyo ambayo imevuja katika baadhi ya
mitandao, Jokate alisema alivalia mavazi hayo hivi
karibuni Afrika Kusini alipokuwa
amekwenda kurekodi wimbo wake mpya
(hakuutaja jina) na alivaa makusudi ili
kuonesha utofauti.
“Nimeamua tu kuwa tofauti maana hata
watu wengi walikuwa wakijiuliza
kulikoni mimi kuvaa hivyo lakini mimi
nafikiri lazima kuna wakati tunatakiwa
kuonekana tofauti na siyo mapambo
muda wote ukibadilika hata unachofanya unakuwa tofauti,” alisema Jokate.
Chapisha Maoni