0
Staa wa Bongo Fleva aliyeiwakilisha Bongo kwenye Shindano la Big Brother Africa 2013 ‘The Chase’, Feza Kessy.


Habari mbaya! Mpenzi msomaji tunasikitika kukujuza kwamba ile ndoa iliyosubiriwa kwa hamu kubwa imeyeyuka baada ya uchumba wa staa wa Bongo Fleva aliyeiwakilisha Bongo kwenye Shindano la Big Brother Africa 2013 ‘The Chase’, Feza Kessy na jamaa kutoka Botswana, Oneal umeanguka chali.

Habari za uhakika zinadai kwamba mwanadada huyo ndiye aliyeamua kukata mzizi wa fitina na kuachana na mwanaume huyo ambaye alitimba
Bongo kumchumbia baada kuona hana mipango ya maisha ya baadaye huku jamaa akiwa bize na maisha yake na mwanaye mwenye umri wa miaka
nane.

Akizungumzia ishu hiyo, Feza alisema: “Mimi ndiye niliyemuacha. Nilitangaza kupitia Twitter (mtandao) lakini ujumbe umefika. Ni kweli tumeachana lakini siwezi kuzungumza in details
(kiundani). Vitu vingine vitafunguka baadaye.

Chapisha Maoni

 
Top