0
KAMA ni mgonjwa, sasa kapona. Hivyo ndivyo unavyoweza kusema, baada ya Manchester United kushinda mechi ya nne mfululizo Ligi Kuu ya England usiku.

Timu hiyo ya kocha Mholanzi, Louis Van Gaal imeshinda mabao 2-1 Uwanja wa Old Trafford dhidi ya Stoke City na kurejea nafasi ya nne katika msimamo wa Ligi Kuu.

Marouane Fellaini aliifungia Manchester United bao la kwanza dakika ya 21 kwa kichwa, kabla ya Steven Nzonzi kuisawazishia Stoke kwa shuti la mbali dakika ya 39 na Juan Mata kuwafungia bao la ushindi wenyeji kwa mpira
wa adhabu dakika ya 59.

United leo iliwakosa nyota wake majeruhi Wayne Rooney na Angel di Maria, na kwa ushindi huo ni dalili kwamba Van Gaal anaelekea kuanza ‘kupunga upepo’ Old Trafford.

Kikosi cha Manchester United kilikuwa; De Gea, Valencia, Smalling, Rojo, Young, Fellaini, Carrick, Herrera/Fletcher dk86, Mata, Van  Persie na Wilson/Falcao dk78.

Stoke City; Begovic, Bardsley, Shawcross, Wilson, Pieters, Cameron, Nzonzi, Ireland/ Arnautovic dk82, Krkic, Assaidi/Crouch dk77
na Diouf.

Chapisha Maoni

 
Top