0

Jumapili ya Des 7 ni siku iliyochukua headline kwenye mitandao baada ya Davido kuwakwaza watanzania kwa kile alichokiandika kwenye
twitter.Baada ya Mwakilishi kutokea Tanzania Idris Sultan kutangazwa kuwa mshindi wa Big Brother
Africa Hotshots.

Mengi yamezungumzwa na watu,lakini Des 11 mshindi wa Big Brother Africa Hotshots,Idris Sultan alipata nafasi ya kuzungumza na vyombo
vya habari mbalimbali. Miongoni mwa maswali aliyouliza ilikuwemo ile ishu ya Davido.

Mwandishi: Idris ukiwa kama mshindi wa BBA unazungumziaje ujumbe wa Davido uliowakwaza watumiaji wa mitandao?
Idris Sultan: " Kwanza ningependa kusema nahisi ilikuwa ni utani kwasababu mwishoni mwa ile
sentensi kumbuka kuna alama ya utani yaani ‘Lol’ sasa nimeshangashwa kuona watu wanaanza kuhisi vibaya kuwa ni dongo kwetu hapana.

"Ningewataka watanzania pamoja na Davido tusiingie kwenye migogoro isiyokuwa na msingi
sisi sote ni bado vijana tunatakiwa kujitangaza na kupeana support hata vizazi vinavyokuja vijifunze
vitu vizuri kutoka kwetu ikiwemo Upendo na Amani kati ya Tanzania na Nigeria."
Hizi ni baadhi ya picha kutoka kwenye mkutano huo

Mshindi wa Big Brother 2014,Idris Sultan
akisisitiza jambo wakati akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) katika hoteli ya Hyatt Regency,Jijini Dar es salaam .

Meneja Uhusiano wa Kampuni ya MultiChoice Tanzania,Barbara Kambogi akizungumza jambo
wakati wa Mkutano na Waandishi wa Habari jijini
Dar es Salaam .

Chapisha Maoni

 
Top