0
Mkuu Mpya wa mkoa wa Mwanza, Magesa Mulongo, amelitaka jeshi la polisi mkoani Mwanza kutotumia nguvu pamoja na kufurumusha mabomu ya machozi kuwatimua wafanyabiashara
ndogondogo maarufu kama machinga mara wanapoombwa na halmashauri ya jiji bila kupata maelekezo.

Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kuhitimisha ziara yake ya ghafla katika wilaya ya Nyamagana, Mulongo amesema kamanda wa
polisi wa mkoa huo, hatakiwi kuruhusu polisi wake kuwafyatulia mabomu machinga huku viongozi wa jiji wakiwa wamekaa ofisini bila kujishughulisha kusikiliza malalamiko
yanayowakabili.

Aidha, Mulongo ameutaka uongozi wa
halmashauri ya jiji la Mwanza kuhakikisha tatizo la uchafu linamalizwa ili kuliweka jiji hilo katika
hali ya usafi zaidi.

Pia mkuu wa mkoa huyo amemtaka afisa afya wa jiji, Danford Kamenya na mwenyekiti wa kikosi kazi cha usafi wa jiji, Kaobwe Phidelis, kufanya mazungumzo ya amani na wafanyabiashara ndogo ndogo na kuwatafutia maeneo yaliyoboreshwa.

Chapisha Maoni

 
Top