0
Mshambuliaji Mpya wa timu ya Yanga,
Danny Mrwanda amevunja ukimya kwa
kusema hakutaka kusajiliwa Simba kwa
mali kauli anachoangalia na 'njuru'.
Mrwanda ambaye ameanza mazoezi na
Yanga jana jioni na kukabidhiwa jezi
namba 24 alisema walishindwana dau na Simba hivyo anaangalia kwenye maslahi.

"Mpira ni kazi yangu, naishi kwa ajili ya
kutegemea mpira, sasa wao wameleta longo longo, Yanga wamekuja nikawapa dau wakakubali nikasaini mkataba, sasa hivi maisha yangu ni Yanga na akili zangu naelekeza kwenye timu yangu mpya na si
mambo mengine, ninachangamoto ya
kuhakikisha Yanga hawajuti kunisajili.
Kuhusu kusaini mkataba wa miezi sita
Simba kama kocha wa wekundu hao wa
Msimbazi Patrick Phiri alivyowahi kusema
wiki iliyopita alisema "Nilifanya
mazungumzo na Simba, na Phiri ananitaka hata leo hii, lakini viongozi wake longo longo, wanataka kunipa hela wanayotaka wao, hapo ndio tumeshindwana."alisisitiza
Mrwanda huku akigoma katu katu kutaja
kiasi alichoitaji Simba wakashindwa
kumpatia.

Hata hivyo Mrwanda alisema kuwa
mkataba wake wa Polisi Morogoro ambayo
inadai Yanga imemsajili mchezaji huyo
kinyemela alisema "Habari za mkataba
wangu na Polisi nisingependa
kuzungumzia, viongozi wa Yanga
watamalizana wenyewe na Polisi."alisema.

Naye kocha wa Yanga Mbrazil Marcio
Maximo alisemaa ameshafanya kazi na
Mrwanda wakati akiinoa timu ya Taifa,
Taifa Stars, anamjua vizuri Danny na
anajua ni kitu gani anaweza kukipata
kutoka kwa mchezaji huyo.

"Mrwanda ni mshambuliaji mzuri ana
uwezo wa kumiliki mpira, kukimbia katika nafasi, kufunga na kupiga pasi. Ingawa
Danny ana udhaifu wake, hasa kuinama
sana chini, ninalitambua tatizo hilo na
nitalifanyia kazi, naamini ataifanya safu
yangu ya ushambuliaji iwe yenye kasi zaidi.

Katika mazoezi ya jana jioni, Maximo
aliweka wazi kikosi chake cha kwanza
ambacho kitaanza katika mechi ya Nani
mtani Jembe dhidi ya mahasimu wao Simba
ambapo langoni alisimama Deogratius
Mushi 'Dida' Juma Abdul, Oscar Joshua,
Kelvin Yondani, Nadir Haroub 'Canavaro'
Mbuyu Twite, Simon Msuva, Emerson de
Oliveira Neves Roque, Hamis Kiiza, Haruna Niyonzima na Andrey Coutinho.

Katika mazoezi hayo ambayo Maximo
alitumia mfumo wa 3-4-3 huku wapiga
penati katika kikosi hicho ni Canavaro,
Msuva, Ngassa, Joshua na Mrwanda, kwa maana hiyo, katika mechi hiyo ya Jumamosi Ngasa na Mrwanda wataingia wakitokea benchi na kuchukua nafasi ya Hamis Kiiza
na Andrey Countinho .

Chapisha Maoni

 
Top