0
Johnson Lukaza na mdogo wake Mwesigwa Lukaza wakiwa mahakamani wakisubiri hukumu


Dar es Salaam. Mahakama ya Hakimu
Mkazi Kisutu imemuachia huru Johnson
Lukaza na mdogo wake Mwesigwa
Lukaza baada ya kuwaona hawana hatia
katika kesi ya wizi wa wa Sh 6.3 bilioni
za akaunti ya madeni ya Nje (EPA) iliyopo Benki Kuu ya Tanzania (BoT).

Akitoa hukumu hiyo jana Kiongozi wa
jopo la Mahakimu watatu wanaoisikiliza
kesi hiyo, Jaji wa Mahakama Kuu, Edson
Mkasimongwa alisema baada ya kupitia
ushahidi uliotolewa na mashahidi saba
wa upande wa mashtaka na utetezi wa
washtakiwa hao anaona upande wa
mashtaka umeshindwa kuthibitisha
mashtaka pasipo kuacha shaka.

Mashtaka matano yaliyokuwa
yakiwakabili hao ni pamoja kula njama,
kughushi, kuwasilisha hati za uongo za
makubaliano ya kuhamisha deni kati ya
kampuni yao ya Kernel Ltd na kampuni
Marubeni ya nchini Japan na kujipatia
kiasi hicho cha fedha cha Sh 6.3 bilioni
kwa njia ya udanganyifu.

Akisoma hukumu hiyo, Jaji
Mkasimongwa amesema wamewaachia
huru washtakiwa hao katika makosa
hayo yote kwa sababu ushahidi wa
upande wa mashtaka haukujitosheleza
kwa kuwa ulishindwa kuthibitisha kama
ni kweli Novemba 2,2003 washtakiwa
hao walighushi hati ya makubaliano ya
kuhamisha deni la Sh 6.3 bilioni baina
ya kampuni ya Kernel Ltd na Marubeni
ya nchini Japan ilikuwa ni ya kughushi.

Jaji Mkasimongwa anasema ushahidi
unaonesha kampuni hiyo ya Marubeni ya nchini Japan ilikubali kupokea kiasi hicho cha fedha na kwamba washtakiwa wao walipata asilimia tu ya 20 ya fedha hizo na upande wamashtaka hakuwahi
kulibishia hilo.

Katika kesi hiyo, Johnson Lukaza ambaye ni Mwenyekiti wa makampuni ya Proin na ni Mjumbe wa Baraza la Chuo Kikuu cha Bagamoyo (UB) pamoja na mdogo wake Mwesiga walikuwa wanatetewa na Wakili Alex Mgongolwa aliyekuwa akisaidiwana na Wakili Alex Mshumbusi.

Baada ya hukumu hiyo kutolewa ndugu
wa washtakiwa hao waliaza kulia
mahakamani hapo pamoja na mshtakiwa Mwesiga wakiwa hawa amini
kilichotokea huku wakisema asante Yesu, asante Yesu.

Chapisha Maoni

 
Top