MKAZI wa kijiji cha Chibwechangula –Behelo katika wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma, Ruth Matonya (26) amejifungua mtoto wa ajabu ambaye
nusu ya sura yake inafanana na binadamu na nusu ikifanana na chura.
Mtoto huyo alizaliwa Desemba 2, mwaka huu katika Kituo cha Afya cha Mtakatifu Luka kinachomilikiwa na Kanisa la Anglikana, Dayosisi ya Mpwapwa. Alifariki dunia muda mfupi baada ya
kuzaliwa.
Kwa mujibu wa Mganga Mfawidhi wa kituo hicho, Dk Edwin Kihura mara baada ya mama huyo kufika katika kituo hicho cha afya alikuwa na uchungu ambao haukuwa na kikomo, lakini alishindwa kujifungua kwa njia ya kawaida licha
ya njia ya uzazi kufunguka.
Alisema kutokana na hali hiyo iliwalazimu kumfanyia upasuaji mama huyo kwa lengo la kuokoa maisha yake na mtoto.
Alisema wakati mama huyo akihudhuria kliniki walipojaribu kupima miezi ya mwisho mama huyo, mkao wa mtoto ulikuwa haupatikani pamoja na
mapigo ya moyo lakini mtoto alikuwa anacheza tumboni jambo ambalo lilikuwa likiwashangaza waganga na wauguzi kituoni hapo.
Dk Kihura alisema mara baada ya mama huyo kufanyiwa upasuaji waliweza kutoa mtoto wa jinsi ya kike ambaye alikuwa na sura isiyoeleweka na kichwa kilikuwa na sura ya binadamu na nusu ikiwa ni sura inayofanana na chura huku viungo
vingine vyote vya mwili vikiwa kamili.
Alisema zipo sababu kadha zinazoweza
kusababisha tatizo kama hili ambapo alisema kuwa ni baadhi ya akinamama kukosa baadhi ya madini mwilini na uumbaji kutokamilika kutokana
na sababu za kibaiolojia.
Alieleza kuwa hali ya mama huyo inaendelea vizuri na kwamba mtoto huyo alikuwa ni mtoto wake wa tano.
Chapisha Maoni