0
Moja ya habari ambazo zilichukua uzito wa juu katika vyombo vya habari wiki iliyopita ilikuwa ni kitendo cha yule mama mfanyakazi wa Chama cha
Republican Marekani, Elizabeth Lauten ambaye alikuwa kitengo cha Mawasiliano kukosoa mavazi ya watoto wa Obama. Habari hiyo bado ni story
inayoendelea kuzungumziwa na sasa
imechukua sura mpya.

Mama huyo aliwaponda Sasha na Malia kuwa wamekosa ustaarabu kutokana na kuvalia sketi fupi katika hafla ya chakula katika Ikulu ya White House, pia alisema kuwa watoto hao ni kama hawakuwa na nyuso za furaha kuwa katika hafla
hiyo, ambapo baada ya kushambuliwa na watu kwenye ukurasa wake wa Facebook aliomba radhi, na baadaye akajiuzulu.

Leo ni siku ya tano tangu amejiuzulu lakini habari mpya ni kwamba bado ameendelea kufuatiliwa na vyombo habari, huku wengine wakipiga kambi
nyumbani kwa wazazi wake kuchunguza vitu mbalimbali ikiwemo rekodi ya maisha yake ya utotoni ambapo watu kwenye mitandao ya kijamii wamekosoa kwa kusema hiyo haikuwa ‘big deal’
ya kufanya vyombo vya habari kumfuatilia kiasi hicho.

Chapisha Maoni

 
Top