Jeshi la polisi limeunda timu ya makachero kutoka makao makuu ya jeshi hilo jijini Dar es salaam wakishirikiana na wa mkoa wa Ruvuma
kufanya uchunguzi kuhusiana na tukio la mtu mmoja aliyelipukiwa na bomu maeneo ya majengo mjini songea na kujeruhi askari polisi wawili wakati akijiandaa kuwarushia askari
waliokuwa doria na kisha bomu hilo kumuua mwenyewe.
Hayo yameelezwa na kaimu mkurugenzi wa makosa ya jinai nchini Naibu Kamishna wa Jeshi la Polisi Diwani Athumani aliyewasili mjini Songea kwa helkopta kwa ajili ya tukio hilo
ambalo mtu ambaye hajatambulika, amelipukiwa na bomu na kufariki dunia wakati akijaribu kuwarushia bomu askari waliokuwa doria na kujeruhi askari wawili PC Mselemu na WP Mariamu Lukindo ambaye bado amelazwa
hospitalini Songea.
Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Said Mwambungu aliyemtembelea majeruhi Mariamu Lukindo ameeleza kusikitishwa na tukio hilo ambalo ni la tatu katika mwaku huu likiwalenga askari polisi.

Chapisha Maoni