Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Lazaro
Nyalandu, amesema habari zinazodai kuwa Serikali inataka kuwaondoa wakazi wa zaidi ya 40,000 katika eneo la Loliondo, Ngorongoro mkoani Arusha hazina ukweli wowote.
Novemba mwaka huu, gazeti The Guardian la nchini Uingereza, liliandika habari kuwa serikali ina mpango wa kuwafukuza Wamasai wanaoishi eneo hilo.
Gazeti hilo lilidai kuwa, lengo ni kuwapatia eneo lenye kilometa za mraba 1,500, kampuni ya OBC ya Falme za Kiarabu.
Akizungumza na wananchi wa jamii ya
kimasai wilayani Ngorongoro mwishoni
mwa wiki, Nyalandu alisema habari hizo
hazina ukweli wowote isipokuwa zina lengo la kuchafua taswira nzuri ya nchi yetu kimataifa.
Aliwataka wakazi wa eneo hilo kuishi bila hofu, kwa sababu serikali haina mpango wa kuwaondoa kwenye makazi yao.
“Nami niwahakikishie wanajamii wa
Loliondo, Ngorongoro na wanajamii wote wa kimasai ambao wametishiwa nyau, kuwa serikali ya Tanzania haina mpango wowote wa kumfuata na kumfukuza mtu yoyote,” alisema.Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Lazaro
Nyalandu akijaribu kurusha mkuki
alipotembelea eneo la Loliondo wilayani
Ngorongoro kukanusha uvumi juu ya
kuondolewa kwa Jamii ya Wamasai katika eneo hilo.
Chapisha Maoni