0
Raia wa Pakistan wakiwaombea watoto 140
waliouawa katika shambulizi la kigaidi katika shule moja nchini humo.


Raia nchini Pakistan wanaadhimisha siku tatu za maombolezo kuwakumbuka zaidi ya watu 140 waliouwawa,karibia wote wakiwa watoto katika shambulio lililotekelezwa na kundi la Taliban.

Waziri mkuu Nawaz Shariff ameitisha mkutano wa vyama vyote vya kisiasa nchini humo kujadili vile watakavyoweza kujibu shambulizi hilo la
Peshawar.

Ameelezea shambulizi hilo kuwa janga la kitaifa lililotekelezwa na wakatili.
Mkuu wa jeshi Jenarali Raheel Shariff ameahidi kulipiza kisasi kwa kila tone la damu linalomwagika.

Nchini India ,shule zimenyamaza kwa dakika mbili ili kutoa heshima kwa wale waliouawa.

Chapisha Maoni

 
Top