msamaha kwa viongozi na watendaji
ambao wametajwa kwa namna moja au
nyingine kushiriki katika uchotwaji wa
mabilioni ya fedha katika akaunti ya Tegeta Escrow kitendo ambacho kimesababisha serikali kupoteza mabilioni ya fedha kama
kodi.
Naibu Waziri wa fedha Mh Mwigulu Nchemba ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu wa CCM Tanzania Bara, amesema hayo mjini Musoma wakati akihutubia mkutano wa hadhara baada ya kuwaapisha makamanda na manaibu makamanda wa umoja wa
vijana wa CCM wilaya na mkoa wa Mara,
ambapo amesema lazima hatua kali za
kinidhamu, kimaadili na kisheria zichukuliwe kwa wahusika wote kama ilivyoazimiwa na bunge la jamhri ya muungano wa Tanzania.
Hata hivyo Naibu huyo Waziri wa Fedha
amekiri kuwa katika zoezi la ubinafsishaji wa mashirika ya umma hasa katika sekta ya viwanda serikali ilifanya makosa makubwa
katika zoezi hilo kwa kuwapa watu ambao wengi wao wamekiuka mikataba ya uendeshaji wa viwanda hivyo hatua ambayo imesababisha viwanda vingi kushindwa kufanya kazi na kufanya vijana wengi sasa kukosa ajira huku serikali ikikosa kodi kupitia
viwanda hivyo.
Kwa upande wake mjumbe wa halmashauri kuu ya taifa wa Chama Cha Mapinduzi Vedastus Mathayo, ameishukuru serikali kwa kukubali kutekeleza mradi wa maji wenye
thamani ya zaidi ya bilioni 50 ambao
amesema kukamilika kwake kutaondoa kabisa tatizo la maji kwa manispaa ya Musoma pamoja na kukubali kugharimia ujenzi wa hospitali ya rufaa ya mkoa wa Mara katika eneo la Kwangwa
Chapisha Maoni