Takribani watu 36 wanahofiwa kufariki katika shambulio lililotokea kwenye machimbo ya kokoto karibu na mji wa Mandera kaskazini mwa Kenya.
Shirika la Msalaba Mwekundu nchini Kenya limethibitisha. Wakazi wa eneo hilo wamesema waathirika wote
wa tukio hilo ni watu wasio Waislam ambao walikuwa wakifanya kazi katika machimbo hayo yaliyopo Kormey kilomita 15 kutoka mji wa Mandera Kaskazini mwa Kenya.
Tukio hili linafuatia tukio la wiki moja iliyopita ambapo watu wapatao 28 waliuawa katika shambulio la basi la abiria huko Mandera.
Kundi la wapiganaji wa Kiislam la Al Shabab limekiri kuhusika na mauaji hayo.
Chapisha Maoni